YANGA SASA YAPANIA MECHI YAO NA LIPULI JUMAPILI

BAADA ya mechi ya juzi dhidi ya Simba, kikosi cha timu ya Yanga kimehamishia nguvu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli ya Iringa ambao unatarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii.

Lipuli imepanda daraja na ratiba inaonyesha watacheza na mabingwa hao wa Ligi Kuu bara kwa mara tatu mfululizo, Yanga katika mchezo wao wa kwanza.

Beki mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema kuwa hawaoni haja ya kuongelea mchezo uliopita na badala yake akili yao wameipeleka katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwasababu lengo ni kuhakikisha wanatetea taji hilo.

“Hakuna timu ndogo katika Ligi Kuu na wala hatuwezi kuingia kwa dharau kwasababu mpango wetu ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine,” alisema beki huyo.


“Tumekaa pamoja kwa muda mrefu, nadhani hakuna sababu ya kutufanya tushindwe kutetea taji hilo, tulipobeba mara ya tatu ilishangaza sasa tunahitaji kufanya kitu kikubwa zaidi,” aliongeza.

No comments