ZANZIBAR STARS KAMBINI CCM MWINJUMA MWANANYAMALA

KATIKA kuhakikisha kuwa wanazidi kujiweka katika ubora wao, Zanzibar Stars Modern Taarab ‘Watoto wa Pwani’ wameanza mazoezi makali yatakayorindima kila Jumatatu, ndani ya CCM Mwinjuma, Mwananyama, jijini Dar es Salaam.

Bosi wa Zanzibar Stars, Juma Mbizo amesema kuwa wameamua kuanza mazoezi hayo ili kujiweka fiti zaidi kutokana na kwamba wana utitiri wa nyimbo zinazohitaji kukumbushiwa kwa sababu ni za muda mrefu.

“Baadhi ya waimbaji wangu wamesahau mashairi ya nyimbo kadhaa, hivyo tumeanzisha mpango huu wa mazoezi ya kila Jumatatu ili waweze kujikumbushia kwa wepesi zaidi,” amesema Mbizo.


Amesema, wakiwa wanaendelea vyema na shoo yao ya DDC Kariakoo kila Jumanne, wamefungua milango pia kwa mapromota wanaoihitaji bendi kwa ajili ya kutumbuiza sehemu mbalimbali ambapo wanaweza kukutana nae ana kwa ana au kumcheki kwenye simu yake ya mkononi.

No comments