ZANZIBAR STARS WAANIKA RATIBA YAO SIKUKUU YA EID EL HAJJ

ZANZIBAR Stars Modern Taarab imetangaza ratiba yake ya maonyesho katika shamrashamra za Sikukuu ya Eid El Hajji ambapo siku ya Idd Mosi watakuwa Tanga Motel, jijini Tanga kwa kiingilio cha sh. 10,000.

Bosi wa Zanzibar Stars, Juma Mbizo amesema kuwa Idd Pili bendi yake itamwaga burudani kwenye kiwanja cha maraha cha Dar Live, Mbagala Zakheem ambapo kiingilio chake kimepangwa kuwa sh. 7,000.

“Septemba 3, mwaka huu tutaunguruma tena Dar Live ambapo tutakuwa tukimsindikiza Christian Bella na Malaika Music Band, huku Dullah Makabila, Pam D na MC Dalada wakialikwa kunogesha,” amesema Mbizo.


Mbizo amesema kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanakonga kisawasawa nyoyo za mashabiki watakaohudhuria shoo zao zote hizo, kwa kumwaga burudani itakayoacha simulizi. 

No comments