ZIDANE AKERWA NA KAULI YA JOSE MOURINHO JUU YA GARETH BALE


Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameonyesha kukerwa na kauli ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho juu ya mshambuliaji Gareth Bale.

Wakati Manchester United na Real Madrid zikitarajiwa kuumana leo usiku katika mchezo wa fainali ya Super Cup inayokutanisha bingwa wa Champions League na Europa League, makocha wa timu hizo wameingia kwenye vita vya maneno.

Majuzi Mourinho alisema anaweza akafikiria kumsajili Bale iwapo hatachezeshwa kwenye mchezo huo wa Super Cup.

"Kama Bale atacheza, basi bado atakuwa kwenye mipango ya timu, lakini wasipomchezesha itatoa picha kuwa hana umuhimu kwao na ninaweza kufikiria kumsajili," alisema Mourinho.

Lakini Zidane amejibu mapigo na kusema Bale ni mchezaji wa Real Madrid na itabaki kuwa hivyo.

"Hatuwezi kushinikizwa na mtu juu ya namna ya kuwatumia wachezaji wetu. Bale ni mchezaji wetu, ni mchezaji muhimu kwetu," alisema Zidane.No comments