Habari

ZIDANE AZIPOTEZEA LAWAMA ZA BENZEMA

on

KOCHA Zinedine
Zidane, amemkingia kifua staa wake, Karim Benzema, baada yakusema kuwa hawezi
kumlaumu kwa kukosa nafasi nyingi katika mchezo ambao Real Madrid waliambulia
sare ya mabao  2-2 dhidi ya Valencia na huku akiyapongeza
mabao mawili yaliyofungwa na nyota wake mwingine,  Marco Asensio.
Katika mchezo huo wa La Liga, Asensio aliweza kuziona nyavu mara
mbili likiwamo bao alilofunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 83 na kuwafanya
mabingwa hao watetezi kuambulia pointi wakiwa kwenye uwanja wao wa Santiago
Bernabeu.
Pamoja na kuambulia pointi, lakini Benzema alipoteza nafasi
nyingi ambazo zingewapa ushindi ikiwamo aliyoipata baada ya  Asensio
kusawazisha, lakini mpira aliojitwisha kwa kichwa ukaishia kugonga mwamba.
Hata hivyo, akizungumza mbele ya waandishi wa habari mara baada
ya mtanange huo, Zidane ambaye kwa ujumla alionekana kupagawa baada ya Benzema
kupoteza nafasi hizo alisema: “Mashabiki wanaweza kufanya chochote kile
wanachokitaka. Lakini jambo la muhimu  Karim alipata nafasi na
amefanya kazi.
“Usiku wa
leo (juzi) hakuweza kufunga, lakini hilo si tatizo. Tumebaki tukitabasamu kwa
sababu hili ni soka,” alisema kocha huyo.

Alisema kwamba, wakati mwingine mambo huwa yanagoma kwenda,
lakini unapaswa kuwa mvumilivu na akasema kuwa hawawezi kukerwa na kile ambacho
mashabiki wanakifikiria.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *