50 CENT AGEUKIA KOMEDI NA KUFURAHIA MAISHA


RAPA wa Hiphop ambaye ni memba wa kundi la G Unit, 50 Cent, amesema kuwa hivi sasa anajisikia furaha kujihusisha na masuala ya komedi.

Rapa huyo ambaye aliwahi kuwa na bifu na Ja Rule, amekuwa akifanya maonyesho ya vichekesho kwenye kumbi mbalimbali nchini Marekani.

“Tunajaribu kuonyesha kitu kingine tofauti ambacho tunaweza kukifanya tukiwa kama kundi, komedi pia ni kitu cha kufurahisha jamii,” alisema rapa huyo.


Rapa huyo alifanikiwa kuteka soko kwa kibao chake cha “In Da Club” miaka ya nyuma, lakini hivi sasa ni kama ameanza kupotea.

No comments