ABDI KASSIM BABI AMUONYA KOCHA WA SIMBA MATARAJIO YA UBINGWA

KOCHA wa timu ya Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon amepewa onyo na aliyekuwa kiungo wa Yanga, Abdi Kassim Babi kuwa asijidanganye kwamba kikosi chake kinaweza kubeba ubingwa kirahisi msimu huu.

Babi amesema kwamba kikosi cha Yanga kinaweza kufanya yale yaliyotokea msimu uliopita ambapo bila kutarajia kikatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

"Omog  asijidanganye na ukubwa wa majina ya mastaa wake kwasababu ukikitazama kikosi cha Yanga kinaonekana kimetimia zaidi kuliko Simba kwani mpaka hivi sasa hakuna mchezaji hata mmoja aliyejihakikishia namba," alisema Babi.


‘’Najua mitazamo ya wengi ni Simba kuwa bingwa mpya lakini wanasahau wastani wa umri wa wachezaji Simba ni mkubwa sana hivyo wanaweza kuchoka haraka Ligi itapochanganya," aliongeza.

No comments