AGUERO NA JESUS 'PACHA' HATARI ZAIDI PREMIER LEAGUE


Wakati hapo mwanzo ilihofiwa kuwa mmoja wao angeusugua benchi, hatimaye imebainika kuwa washambuliaji Sergio Aguero na Gabriel Jesus wa Manchester City ndio pacha hatari zaidi Premier League.

Washambuliaji hao kutoka Brazil na Argentina wamekuwa wakifunga katika kila mechi tangu msimu huu uanze huku wakionyesha maelewano ya hali ya juu uwanjani.

Aguero ambaye ndiye aliyekuwa hatarini zaidi kupoteza namba, ameonyesha kuwa hana hiyana na mshambuliaji mwenzake ambapo mara kadhaa amekuwa akimpa pasi safi za mwisho.

Wakati City ikiichapa Liverpool 5-0 kwenye Premier League, Aguero aliwaduwaza wengi baada ya kupewa pasi ya mwisho na Fernandinho, lakini badala ya kufunga, naye akatoa pasi kwa Jesus aliyekuwa yeye na wavu, akafunga kirahisi.


No comments