AJIB ACHEKELEA MWANZO WAKE MZURI YANGA SC

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amesema anafurahi kuanza vizuri kuchezea timu yake hiyo mpya na kwamba bao alilofunga litamwongezea ari ya kufanya vyema kwenye mechi zinazokuja.

Ajibu amesema kuwa, lengo lake ni kuona kuwa mabao anayofunga yanaisaidia Yanga kufanya vizuri katika mashindano yote ambayo watashiriki msimu huu hivyo amejiandaa kwa mapambano.

“Nipo sawa ukilinganisha na mwanzo. Napenda kufunga mabao sio kwa sababu yangu bali ni kwa sababu nataka kushinda kitu nikiwa na Yanga,” alisema Ajibu.

“Kufunga kila mshambuliaji anaweza kufanya hivyo lakini ni kwa kiasi gani mabao yamechangia kupatikana kwa ubingwa, hicho ndio kitu bora zaidi,” aliongeza.


Ajibu amesema anahitaji kufanya vyema na kuonyesha kiwango kikubwa tofauti na wakati alipokuwa na wekundu wa Msimbazi.

No comments