ALICIA KEYS AGUSWA NA WAATHIRIKA WA KANSA MAREKANI, AAMUA KUWASAIDIA

STAA mwenye mvuto, Alicia Keys ameanza kufanya kampeni za kusaidia waathirika wa matatizo ya kansa za matiti nchini Marekani.

Nchini Marekani tatizo hilo la kansa ya matiti limeongezeka kwa asilimia 42 ambapo namba hiyo kwa kiasi kikubwa imeangukia kwa wanawake weusi wenye asili ya Kiafrika.

Katika kampuni hiyo ameungana na Ophelia ili kutunisha mfuko wa kansa na kugharamia wanawake ambao wameathirika na tatizo hilo.


“Nimekulia Harlem, sehemu ambayo tatizo hili ni kubwa sana, nina kila sababu ya kusaidia wanawake wenzangu ambao wamekumbwa na janga hili,” alisema Keys.

No comments