ALICIA KEYS AWAPONDA MADEMU WA KIMAREKANI AKISEMA HAWAJIAMINI

ALICIA Keys, staa anayetajwa kuwa na mvuto wa kimapenzi nchini Marekani amesema kuwa wanawake wengi wa taifa hilo hawajiamini kiasi cha kutumia gharama kubwa ili kubadilisha mionekano yao ya asili na kuwavutia wanaume.

Mrembo huyo mwenye miaka 36, ameliambia jarida la Elle kuwa ataendelea na kampeni yake ya kubadilisha mitazamo ya wanawake ili kuwajengea hali ya kujiamini wakiwa na mionekano yao ya asili.

“Hakuna maana yoyote kutumia gharama kubwa kwa sababu ya kubadilisha maumbile, wanawake wanapaswa kujiamini vile walivyo,” alisema Keys.


“Nitaendelea na kampeni hii ili kuokoa ustawi wa wanawake kuondokana na dhana potofu ya kujiona hawafai mbele ya jamii mpaka wabadilishe maumbile,” aliongeza.


No comments