ALLY AKIDA NA BENDI YAKE YA TOP STARS APATA MWALIKO MSUMBIJI


Ally Akida mcharaza gitaa la solo na rhythm aliyepata kutamba na Twanga Pepeta, amepata mwaliko wa kufanya maonyesho nchini Msumbiji.

Akiongea na Saluti5, Ally Akida amesema yeye na bendi yake ya Top Stars yenye maskani yake Songea, wataondoka tarehe 27 mwezi huu kwa ziara ya wiki mbili.

Tulo, Dapol na Beira ni miongoni mwa miji itakayopiga Top Stars ambayo inaundwa na wasanii kama Wakuziba, Rojaz, Bob Kisa na mwimbaji wa kike Nana.

No comments