Habari

ANTONIO CONTE HANA MPANGO WA KUFUNDISHA NJE YA ITALIA KWA MUDA MREFU

on

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesisitiza kuwa siku moja atarejea kufundisha nyumbani kwao Italia. 
Conte alitua  Stamford Bridge mwaka 2016 na kupata mafanikio ya haraka kwa kuitoa timu kwenye nafasi ya 10 iliyomaliza msimu mmoja kabla ya utawala wake hadi kutwaa taji la Premier League.  
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Conte mwenye umri wa miaka 48 kufanya kazi nje ya Italia akiwa amezikochi Arezzo, Bari, Atalanta, Siena, Juventus na timu ya taifa ya nchi hiyo.
Conte pia alitumia maisha yake ya kusakata kandanda Italia kwa kuanzia Lecce kabla ya kuichezea Juventus kwa miaka 13 na sasa ana matumani makubwa ya kurejea Serie A.
Akiongea na Radio Rai ya Italia, Conte alisema: “Nimekumbuka sana Italia. Ndani ya kichwa changu sina fikra za kukaa nje kwa muda mrefu.
“Mara nitakapojiongezea uzoefu nitarejea Italia, hilo halina shaka. Sijui ni lini lakini hilo ni lengo langu kuu.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *