ARSENAL 'WAZEE WA ALHAMISI' WAANZA NA MKWARA MZITO EUROPA LEAGUE ...Everton na Rooney wake hoi


Arsenal imeanza kwa kishindo michuano ya Europa League baada ya kuitungua Colgne ya Ujerumani 3-1 ndani ya dimba la Emirates ambalo lilitawaliwa na vurugu nyingi za mashabiki wa Colgne waliosafiri na timu hadi London.

Jhon Cordoba alikuwa wa kwanza kuitanguliza Colgne kwa kuifungia bao la kuongoza dakika ya 9 ambalo lilidumu hadi dakika ya 49 pale wenyeji waliposawazisha kupitia kwa beki wa kushoto Sead Kolasinac.

Kolasinac alifunga bao hilo kwa shuti kali dakika nne tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Rob Holding.

Mshambuliaji Alexis Sanchez akafunga bao lake la kwanza msimu huu dakika ya 67 kabla Hector Bellerin hajahitimisha ushindi kunako dakika ya 81 kwa kuifungia Arsenal bao la tatu.

Arsenal (3-4-3): Ospina 5; Holding 5 (Kolasinac 45, 7.5) Mertesacker 6, Monreal 6.5; Bellerin 7.5, Iwobi 6.5 (Wilshere 68, 6.5), Elneny 6, Maitland-Niles 6; Walcott 6 (Nelson 82), Giroud 6.5, Sanchez 7
Wafungaji: Kolasinac 49, Sanchez 67, Bellerin 81

Cologne (4-1-4-1): T. Horn 6; Klunter 6 (Osako 78), Mere 7, Heinz 6, Rausch 5.5; Lehmann 6.5; Zoller 5 (Risse 65, 6), Hoger 5.5, Hector 5.5 (Jojic 35, 5.5), Bittencourt 6; Cordoba 7
Mfungaji: Cordoba 9

Wakati Arsenal ikivuna ushindi huo mnene, klabu nyingine ya England, Everton ikiwa na Wayne Rooney ikachapwa na Atalanta ya Italia 3-0 katika michuano hiyo ya Europa League ambayo huchezwa siku za Alhamisi.
No comments