ARSENAL YAINYUKA WEST BROM 2-0 … Alexandre Lacazette moto chini


Alexandre Lacazette ameendelea kuonyesha ubora wake kwa kuifungia Arsenal mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la Emirates, Lacazette alifunga goli la kwanza dakika ya 20 kabla ya kupachika la pili kwa mkwaju wa penalti kunako dakika ya 67.

No comments