ARSENE WENGER AOMBA 'PO' KWA MASHABIKI WA ARSENAL


ARSENE WENGER amewataka mashabiki wa Arsenal wasife moyo na mwanzo mbovu wa msimu huu na badala yake waibebe timu kwa kuiunga mkono.

Arsenal imesajili wachezaji wawili tu kiangazi hiki Alexandre Lacazette na Sead Kolasinac huku wakishindwa kumsajili Thomas Lemar licha ya kuweka pauni milioni 92 siku ya kufunga dirisha la usajili.

Hata hivyo, Wenger amesema licha ya usajili huo mdogo, lakini mafanikio yanaweza kupatikana kwa mashabiki kuiunga mkono timu - ila Arsenal itaanguka iwapo mashabiki watakwenda kinyume dhidi yao.

"Watu wanabadilika haraka sana na unasahau ubora ulionao - wana maamuziki ya haraka kuliko unavyofikiri," Wenger aliiambia beIN SPORTS.
“Tunapaswa kuendelea kuamini uwezo na ubora wetu na si kuusahau.  Ili kuwa na msimu mzuri, tunahitaji 'sapoti' ya mashabiki wetu".
No comments