ATHUMAN KAMBI AWATAKA AKINADADA KUPUNGUZA "SHOBO" KWAKE

MWIMBAJI wa sauti kali ndani ya Msondo Ngoma Music Band, Athuman Kambi amewataka akinadada wanaomsumbua wakimtaka kimapenzi kucheza mbali nae akidai kwamba yeye tayari ni mali ya mtu.

Akiongea na Saluti5, Kambi amesema kuwa amekuwa akikosa raha na amani kutokana na kitendo cha baadhi ya akinadada kumwandama wakihitaji kuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi.

“Mimi tayari ni mume wa mtu jamani, najichunga na hata nyie pia naomba mjichunge, kwasababu naamini wengi wenu mna wapenzi wenu kama ilivyo kwangu mimi vilevile,” amesema staa huyo ambaye hivi sasa anatamba na kibao ‘Heshima Iko Wapi’.


“Nampenda sana mke wangu na naamini hata yeye pia ananipenda, hivyo sitaki kumkosea adabu kwa namna yoyote ile, kwahiyo tafadhali tuheshimiane kwani mnaponighasi mnamfanya akose kujiamini kwa asilimia zote,” ameongeza Kambi.

No comments