Habari

AUDIO: WAZIRI SONYO ATUHUMIWA KUMCHOMA KISU MSANII MWENZAKE, YEYE ASEMA NI CHUPA SIO KISU

on

Mmoja wa waimbaji wenye sauti tamu na waliofanikiwa kuliteka soko la
muziki wa dansi mwanzoni mwa miaka ya 2000, Waziri Sonyo anadaiwa kumchoma kisu
mwimbaji mwenzake Rama Igwe.
Tukio hilo limetokea mjini Arusha wiki iliyopita ambapo kupitia
mtafaruku baina ya waimbaji hao wawili kupitia, ikadaiwa Sonyo akamchoma kisu
mwenzake na kumjeruhi vibaya.
Wasanii wote wawili waliweza kufanya mahojiano na Radio TK FM ya Tanga
kupitia kipindi cha Afro Dance kinachoongozwa na Rajab Mohamed “Rogie Kiss”
ambapo wote walikiri kuwepo kwa tukio hilo.
Wakati Rama Igwe akisema alichomwa kisu, Sonyo amesema sio kisu bali
ni chupa na kwamba alikuwa akijibu mashambulizi ya Rama.
“Rama alinikimbiza hadi kwenye bustani na kunirushia chupa ikanijeruhi
jichoni na mimi nikaishika chupa ile ile na kumpelekea nayo kujibu
mashambulizi,” alisema Sonyo katika mahojiano yake na TK FM.

Isikilize clip yao hapo chini ambapo mwanzo utamsikia Rama Igwe na
kisha mwishoni utamsikiliza Waziri Sonyo kama walivyoongea na TK FM kupitia
Afro Dance.

 Waziri Sonyo
 Rama Igwe alivyokuwa ametota damu
 Rama Igwe alijeruhiwa shingoni na kuvuja damu nyingi

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *