AZAM FC SASA WAPANIA KUIADHIRI SIMBA SC

KOCHA wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kuwa baada ya kuanza vyema kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda hivi sasa wamepania kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi yao na Simba.

Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA Kagame Cup, walizoa pointi zote tatu katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya kuichapa Ndanda bao 1-0 ugenini ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

“Simba ni moja ya timu nzuri wanacheza mpira mzuri na sasa tunasubiri kitakachotokea kwenye mchezo huo, timu yangu malengo yake hivi sasa katika kila mchezo ni kuwa makini na kukusanya pointi nyingi kadiri iwezekanavyo,” alisema.

“Tunajua ubora wao katika safu ya kiungo lakini hakuna namna ni lazima tuingie kwa dhamira ya kuusanya alama tatu katika mchezo huo,” aliongeza.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri kipindi hiki kabla ya kuanza kwa msimu na kikosi kina hali ya ushindi, sioni ni kwa namna gani tunawezea kupoteza hali hii.”


Azam msimu uliopita haukuwa na mwenendo mzuri kwenye michuano ya Ligi Kuu bara baada ya kukosa nafasi za juu, lakini pia waliukosa ubingwa wa Kombe la FA, hivyo kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. 

No comments