Habari

BAADA YA LIVERPOOL KUTOLEWA NA LEICESTER KATIKA EFL CUP …KLOPP ATETEA UAMUZI WA KUMPUMZISHA COUTINHO

on

Kocha wa Livepool Jurgen Klopp ametetea uamuzi wake wa kumpumzisha kipindi cha pili mshambuliaji Philippe Coutinho, lakini akakiri kuumizwa na matokeo ya kipigo kutoka kwa Leicester City kwenye mchezo wa Carabao Cup.
Leicester wakaitupa nje Liverpool kwa kichapo cha 2-0 katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la Carabao, ambayo pia hufahamika kama kombe la EFL kwenye dimba la  King Power.
Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kuondolewa uwanjani.
“Ilikuwa ni mipango yangu tangu mwanzo. Anahitaji kurejea taratibu, sikuwa na fikra za kumchezesha kwa dakika 60, 70 au 80,” anaeleza Klopp
“Dakika 45 ni sahihi. Tunahitaji awe fiti lakini hatuwezi kutumia nguvu kubwa,” aliongeza Klopp.
Bao la kwanza lilifungwa na nyota wa Algeria Islam Slimani huku la pili likifungwa na Shinji Okazaki aliyetajwa kama ‘man of the match’. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *