BM RECORDS STUDIO YAWAITA WASANII KUINGIA "LEBO"

BM Records Studio ya Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salam imeendelea kuwataka wasanii wa miondoko mbalimbali ya muziki kujitokeza Studioni hapo kwa ajili ya kujiunga na lebo yao.

Mkurugenzi wa BM Records, Beatrice Masumbuko ameongea na Saluti5 na kubainisha kuwa, tayari wameanza kupokea maombi kutoka kwa wasanii chipukizi wa maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

“Bado tunawasisitiza wasanii kuzidi kujitokeza kwani tumekusudia kuwa na wasanii wengi zaidi kwenye lebo yetu, hivyo watakaokuwa tayari wanaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0652 585 655 au 0786 966 369,” amesema Beatrice.


“Au msanii anaweza kufika moja kwa moja katika ofisi zetu zilizoko Kigogo Luhanga, jirani na stendi ya mabasi na kupata mikakati yetu kamili ikiwa ni pamoja na kushuhudia namna tulivyojipanga kwa ajili ya kuinua vipaji,” ameongeza mkurugenzi huyo.

No comments