Habari

CHELSEA ‘KUMSAJILI’ ALEX SANDRO WA JUVENTUS MWEZI JANUARI

on

CHELSEA ipo tayari kujaribu tena kumsajili nyota wa Juventus Alex Sandro.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alihusishwa kwa kiasi kikubwa na uhamisho wa kwenda Stamford Bridge dirisha la usajili la kiangazi.
Juve wakakomalia ada ya pauni milioni 60 kwa beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26, lakini Chelsea wakakataa kulipa kiasi hicho cha pesa, hatua iliyomfanya Sandro abakie kwa miamba hiyo ya Italia chini ya kocha Max Allegri.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa Chelsea itajaribu tena kumsajili beki huyo katika usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *