Habari

CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA COSTA KWA PAUNI MILIONI 57 KWA ATLETICO MADRID

on

Chelsea imekubaliana na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa pauni
milioni 57.5 wa mshambuliaji Diego Costa utakaomwezesha mshambuliaji huyo mtukutu
kurejea Hispania na kuichezea timu yake ya zamani.
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye
aliondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa vipimo vya
afya siku chache zijazo.
Hata hivyo hawezi kuichezea Atletico hadi mwezi Januari wakati adhabu
ya klabu hiyo ya kutoruhusiwa kufanya usajili itakapokuwa imemalizika.
Costa raia wa Hispania mzaliwa wa Brazil, alijiunga na Chelsea kutoka
Atletico Madrid kwa kitita cha pauni milioni 32 miaka mitatu iliopita.
Aliifunga mabao 58 katika mechi 120 za Chelsea ikiwemo mechi 10 za Ligi
Kuu ya Englad  msimu uliopita ambapo
Chelsea waliibuka mabingwa

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *