CLEMENT SANGA APANIA MAKUBWA BODI YA LIGI

KAIMU mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amejipima na kuona yuko sawa na sasa ameamua kuchukua fomu za kugombea kuongoza bodi ya soka la Tanzania.


Sanga ambaye akili yake ya kiuongozi inakubalika kwa viongozi wengi wa soka, amechukua fomu hiyo wiki iliyopita na Jumanne jina lake likapita katika wagombea wa nafasi ya mwenyekiti akimvaa kiongozi anayemaliza muda wake, Ahmed Yahya.

No comments