DAVID DE GEA 'AFUTA' NJOZI ZA KWENDA REAL MADRID


DAVID DE GEA ni kama vile ameonyesha dhamira ya kudumu Manchester United kwa muda mrefu baada ya kuhamia kwenye mjengo mpya wa kifahari.
Kipa huyo wa United amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na Real Madrid na inaaminika miamba hiyo ya Hispania ingerejesha tena mawindo yao kiangazi kijacho.
United ilipata mashaka baada ya  De Gea kuipiga bei nyumba yake ya pauni milioni 3.85 mapema mwaka huu ambapo tetesi zikazagaa kuwa hayo ni maandalizi yake ya kurejea Hispania.
Lakini sasa kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid akiwa na kipenzi chake Edurne, amehamia kwenye mjengo mkubwa zaidi na ingawa anaishi kwa kulipa pango lakini inaaminika kuna kipengele cha kulinunua jumla.

No comments