Habari

DIEGO COSTA ALIVYOKATAA OFA YA EVERTON ILI KUTIMIZA NDOTO YA KUREJEA ATLETICO MADRID

on

Inaelezwa kuwa Everton ilijaribu kumsajili Diego Costa kutoka Chelsea ukingoni mwa dirisha la usajili la kiangazi, lakini ikaambiwa mchezaji huyo akili yake ipo Atletico Madrid.
Gazeti la Marca la Hispania linadai ofa ya pauni milioni 66.4 ilitumwa kutoka Goodison Park kwenda Stamford Bridge kwaajili ya mshambuliaji huyo mtata, lakini maofisa wa Everton wakakatishwa tamaa.
Ingwa Chelsea ilitaka kumuuza, lakini Costa alishakataa kusikilizwa kwa ofa zingine isipokuwa ile ya klabu yake ya zamani, Atletico Madrid licha ya ukweli kuwa hataweza kuichezea hadi mwezi Januari.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *