Habari

DIEGO COSTA APATA MAPOKEZI MAKUBWA ATLETICO MADRID, AMPIGA DONGO ANTONIO CONTE

on

Diego Costa amewasili Madrid, Hispania na kupata mapokezi makuwa kwa mashabiki wa Atletico Madrid atakayojiunga nayo rasmi mwezi Januari.
Nyota huo aliyemwagana na Chelsea akampiga dongo la kiaina kocha Antonio Conte wakati akiongea na waandishi wa habari.
Costa akasema: “Sikutaka kuondoka kwa njia hii. Kuna mema mengi niliyoyafanya kwa watu wa Chelsea. Sitaki heshima yangu ndani ya Chelsea ufutike kwa sababu ya mtu mmoja”.
Conte ndiye aliyemkataa Costa  mara tu baada ya msimu kumalizika ambapo alimtaarifu mchezaji huyo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi kuwa hana nafasi tena Stamford Bridge.
Wakati wa maandalizi ya msimu mpya, Costa akagoma kurejea Chelsea na akaendelea kubakia nyumbani kwao Brazil hata pale alipotakiwa kuripoti klabuni wakati suala lake la uhamisho likiendelea kushughulikiwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *