Bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” itaanza kupatikana Bulyaga Bar Temeke kila Jumatano.

Mratibu wa matukio ya burudani ndani ya Bulyaga, Muddy K, ameiambia Saluti5 kuwa FM Academia wataanza kupatikana hapo kuanzia Jumatano ya Septemba 27 na kila Jumatano huku kiingilio kikiwa ni kinywaji chako tu.

Kuwepo kwa FM Academia hapo Bulyaga, kunafanya kuwe na mchuano wa yake kati ya bendi tatu kubwa.

Twanga Pepeta hupatikana hapo kila Ijumaa huku Msondo Ngoma wakipatikana kila Jumapili.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac