Kocha wa Manchester City  Pep Guardiola amesema  Yaya Toure bado hajafanya juhudi zozote mazoezini kuthibitisha kuwa anastahili kucheza japo kwa dakika moja msimu huu.

Guardiola amemuengua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 katika kikosi kitakachoivaa Feyenoord kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano usiku. 

"Anajua kwanini nimemuacha, ni kati yangu mimi na yeye. Ni uamuzi wa kimichezo, nataka makubwa kutoka kwa Yaya, makubwa kutoka kwa kila mchezaji," alisema Pep Guardiola.USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac