HAJI MANARA AJIPANGA KULIPUA BOMU SIMBA SC

AFISA Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, siku yoyote anaweza kulipua bomu ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitesa na kuidhohofisha klabu hiyo kiuchumi.

Kwa muda mrefu sasa Simba imekuwa ikikosa mapato yake kwa mauzo ya jezi yanayofanywa na wajanja wachache, na Manara amesema yupo tayari kuwataja wanachama wa klabu hiyo wanaouza jezi feki kujinufaisha wenyewe bila klabu kupata chochote katika mauzo ya jezi hiyo.

"Klabu ambayo inanilipa mimi mshahara, klabu ambayo inaendesha maisha yangu na ya katibu na watu wengine lakini watu wengine wananufaika."

"Siwezi kukubali, mimi ndio nitakuwa wa kwanza kuwataja wanachama wanaouza jezi feki kwanini tuogope? Tumeajiliwa kulinda brand na maslahi ya klabu  ya Simba na ndicho tutakachofanya.’’

Afisa habari huyo amesema kuwa Simba inauza jezi zake kupitia matawi, maduka tofauti lakini bado wanakabiliwa na wimbi la uuzwaji wa jezi feki.

Manara ameziomba mamraka zinazohusika kuasidia klabu ya Simba kupambana na wauzaji jezi feki jambo ambalo limekuwa likidhohofisha uchumi wa klabu hiyo kwa kiasi kikubwa huku wajanja wachache wakinufaika.


Kama Manara atawataja watu hao atakuwa kiongozi wa kwanza hapa nchini kuamua kujitoa muhanga kupambana na biashara hiyo haramu, ambapo wahuni wachache wamekuwa wakiuza jezi hizo huku klabu ikikosa mapato.

No comments