HALICHACHI Classic Modern Taarab wameingia Studio na kuachia kibao chao kipya kinachokwenda kwa jina la “Sina Jema” ambacho kimeimbwa na staa wao wa kike, Mwanahawa Chipolopolo.

“Sina Jema” ni kete ya pili kwa Halichachi Classic baada ya kibao cha kwanza cha “Tatizo Wazazi” ambacho kiliachiwa hivi karibuni kikiwa kimeimbwa na Chipolopolo pamoja na Omary Sosha.

Akiongea na Saluti5, bosi wa halichachi Classic, Amour Maguru amesema kuwa “Sina Jema” wameurekodia ndani ya Studio ya U &I iliyopo Kimara Kona, jijini Dar es Salaam na kwamba utaanza kupatikana wiki hii kwenye mitandao ya kijamii na radio mbalimbali Bongo.


“Kiukweli hiki ni kibao ambacho sidhani akma kuna mtu atakisikiliza kisha akakitoa kasoro, kwasababu tumejitahidi kutuliza akili na kumaliza ufundi wetu wote katika kukiandaa,” amesifu Amour ambaye ni kati ya wapapasaji kinanda hodari wa taarab.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac