HAMIS KIIZA AMVULIA KOFIA EMMANUEL OKWI

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na Yanga, Hamis Kiiza “Diego” amesema kwamba uwezo wa Emmanuel Okwi unatisha.

Kiiza ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Sudan, amesema kwamba Okwi bado ni mshambuliaji hatari katika ukanda huu na kwamba atakuwa msaada mkubwa kwa Simba.

“Sina mashaka kabisa na uwezo wa Okwi, ni mtu hatari anapokuwa karibu na goli, anajua afanye nini kwa ajili ya timu yake,” amesema Kiiza akihojiwa baada ya matokeo ya timu ya taifa ya Uganda “The Cranes” na Mafarao wa Misri ambao bao la Okwi la dakika ya 51 liliwaondoa Waarabu hao vichwa chini.

Kiiza anayecheza katika timu ya Al Hilal Obeid ya nchini Sudan, amesema kwamba usajili ambao Simba wameufanya ni mkubwa na unaweza kuwapa matunda makubwa pia. 

Lakini amesema kuwa hatua ya kumrejersha Okwi Simba wamelenga kuzifunika timu nyingine nyingi katika ukanda huu.

“Okwi mshambuliaji bora katika ukanda huu na atakuwa na msaada mkubwa sana kwa simba kuhusu na uwezo wake sina cha kuongeza kusema,” amesema Kiiza ambaye aliondoka Simba akiwa mfungaji bora lakini tatizo ni nidhamu ilimfanya akatemwa.


Baada ya kutemwa alikwenda kujaribu maisha katika nchi za Afrika Kusini lakini nako yakawa ni yaleyale na kurejea Uganda ambako alicheza kwa muda kabla ya kupata dili hilo la Sudan.

No comments