HIMID MAO MKAMI AWATAKA SIMBA KUJIANDAA NA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KESHO JUMAMOSI

HIMID Mao Mkami ndiye kiungo anayehofiwa zaidi na washabiki wa Simba tangu alipokatisha ndoto yao ya kubeba kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kupiga shuti kali la kushtukiza  katika mchezo wa fainali.

Nohodha huyo wa Azam FC, ameiambia Simba kuwa wajiandae na kipigo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utapigwa Jumamosi hii.

Himid amesema kuwa mpango wao ni kushinda mechi mfululizo baada ya kuifunga Ndanda FC katika mchezo wa ufunguzi.

"Najua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wetu, hatutishiwi na majina ya wachezaji wa Simba, kitu cha msingi kwetu ni kuendeleza umoja wetu,’’ alisema Himid.

"Makosa tuliyoyafanya msimu uliopita hatuhitaji tena yajitokeze msimu huu, tunajua mkakati wa Omog na kikosi chake cha Simba lakini kwetu hatuwezi kutishwa na lolote, tunawafahamu tumecheza nao kwa mechi nyingi,"’ aliongeza.

Nahodha huyo amesema pamoja na kikosi chao kukosa wachezaji wenye majina makubwa lakini anahamini hakuna kitakachoshindikana kwa sababu soka halichezwi na majina bali ni uwezo wa wchezaji wa timu.

Amesema wachezaji wengi waliosajiliwa na Azam msimu huu hawana majina lakini wana uwezo mkubwa wa kucheza na kuipa matokeo timu, jambo ambalo wanajivunia.

"Tulicheza na timu kubwa kule Uganda kwenye mechi za majaribio wa kujiandaa na msimu huu na tulipata ushindi hivyo Simba hawawezi kututisha,’’ alisema.


Azam imeondokewa na wachezaji wake nyota 8, ambao wane katri yao wamejiunga na Simba nawengine Yanga na Ruvu Shooting lakini hata hivyo wamefanya usajili kuziba nafasi muhimu zilizokuwa zimeachwa wazi.

No comments