IVORY BAND YAENDA KUJICHIMBIA TUNDURU KWA WIKI TATUIvory Band, moja ya bendi za kisasa za muziki wa dansi, imeamua kwenda kujichimbia Tunduru na itakuwa huko kwa muda usiopungua wiki tatu.

Akiongea na Saluti5, mmoja wa viongozi wa bendi hiyo Rama Pentagon, amesema wakiwa huko watakuwa wakitumbuiza ndani ya Club Amazon kila siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

“Tumepata mkataba wa wiki tatu kutumbuiza hapa, lakini pia tutatumia ziara hii kama kambi ya kusuka nyimbo mpya na program mpya ya bendi maana huku kuna utulivu mzuri”, anaeleza Pentagon.

Kiongozi mwingine wa bendi hiyo inayoendelea kutesa na wimbo  mpya “Shika Moyo” ni Saleh Kupaza.


No comments