JADO FFU ASAKA RAFIKI ANAYEWEZA KUPIGANA NA MAISHA

BOSI wa Bendi ya Dar Musica, Jado FFU amesema kuwa mwanaume wa ukweli anatakiwa kujiamini kwanza na awe mtafutaji asiyechoka, kama ilivyo kwa upande wake yeye.

Jado amesema kuwa binafsi anamtanguliza Mungu kwa kila jambo huku akiwa hapendi kukata tamaa kwa maneno ya walimwengu kwasababu anafahamu maisha ni kujua kuwa shida na raha vipo kwa ajili ya kila mtu.


“Kwa kawaida sipendi kupigana na wanadamu, napenda kupigana na maisha yangu na mtu wa namna yangu ndie anayeweza kuwa rafiki yangu bila kujali jinsia yake,” amesema Jado.

No comments