JADO FFU ASEMA “NITAZIDI KUPAMBANA NA HALI YANGU”

BOSI wa Dar Musica, Jado FFU amefunguka na kusema kuwa, pamoja na vikwazo anavyokumbana navyo kadri anavyojitahidi kupiga hatua, lakini atahakikisha hakati tamaa ili kuyafikia kikamilifu malengo aliyojiwekea.

“Namtegemea Mungu wangu katika yote na naamini kuwa yeye ndio wakili wangu wa kweli kwangu mimi mtoto wake, hivyo naahidi kutokata tamaa katika kujihangaisha,” amesema Jado.


“Nitapambana na hali yangu hadi pale pumzi zitakapokatika, naomba sana Mungu anisimamie katika hili,” ameonngeza nguli huyo mwenye sauti tamu ya kuimbia.

No comments