JAHAZI KUNGURUMA AIRPORT LEO USIKU NDANI YA AEROSPACE BAR …wakali wa Vanga kusindikiza


Jahazi Modern Taarab leo usiku watarindima ndani ya ukumbi wa Aerospace Bar ulioko maeneo ya Airport jijini Dar es Salaam.

Kundi hilo litajitosa katika ukumbi huo ambao zamani ulijulikana kama Airline KII’, likiwa na wasanii wake wakali wakiwemo Ally Jay, Jumanne Ulaya, Emeraa Solo, Shamary Zizzou, Mazoea, Prince Amigo, Mwasiti Kitoronto na Mishi Zele.


Kama vile hiyo haitoshi, Jahazi watasindikizwa na wakali wa miondoko ya vanga wanaojiita Vanga la F.

No comments