JAHAZI WAJA NA USIKU WA KUKUMBUKA ZAMANI …Khadija Yussuf, Bi Mwanahawa Ali ndani ya nyumba


Jahazi Modern Taarab, Jumamosi hii itajitosa ndani ya ukumbi wa Dar Live kwa onyesho maalum la kukumbuka zamani ambapo nyota kibao waliopata kuitumikia bendi hiyo watashiriki onyesho hilo.

Mwanamama aliyetamba na nyimbo za “Roho Mbaya Haijengi” na “Wema Hazina kwa Mungu” ndani ya Jahazi, Bi Mwanahawa Ali atakuwepo Dar Live kumimina uhondo wa enzi hizo.

Mwimbaji mwingine anayetajwa kuwepo kwenye onyesho hilo ni Khadija Yussuf “Chiriku” ambaye hii itakuwa ni mara ya kwanza kupanda jukwaa la Jahazi tangu alipojiengua kundini mwaka jana, muda mfupi tu baada ya kaka yake Mzee Yusuf kustaafu muziki.

Saluti5 imehabarishwa kuwa waimbaji Rahma Machupa, Miriam Amour, Fatma Mcharuko na Mohamed Ali ‘Mtoto Pori’ nao pia watakuwepo Dar Live Septemba 16.


No comments