JAMIE REDKNAPP mwanasoka wa zamani wa Liverpool na Tottenham ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka, amesema anaamini Romelu Lukaku atatwaa kiatu cha dhahabu mwezi Mei.

Redknapp amewachambuwa washambuliaji wanne Harry Kane wa Tottenham, Alvaro Morata wa Chelsea, Sergio Aguero wa Manchester City na Lukaku wa United ambao wanaonekana wako kwenye ligi yao yao kuwania ufungaji bora wa Premier League.

Licha ya kusema Harry Kane ni mshambuliaji aliyekamilika zaidi, lakini Redknapp anasema Lukaku anapotumia vizuri nguvu zake, hakuna wa kumzuia kutwaa kiatu cha dhahabu.


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac