JB NAE SASA AUCHOKA "UBONGENYANYA"... atamani kurejea kuwa kimbaumbau

MIEZI michache baada ya mkali wa Bongofleva, Peter Msechu kutangaza kuwa yupo kwenye mkakati wa kupunguza uzito wa mwili wake, nae msanii mwingine wa Bongomuvi, Jacob Stephen "JB" ameibuka na kauli kama hiyo.

Katika posti yake aliyoitoa kwenye ukurasa wa Instagram, JB ameandika “Natarajia kurudi kwenye mwili wangu huu… baada ya miezi 7… karibu kwenye mazoezi maalum ya diet."

“Matayarisho ya muvi mpya, ila baada ya filamu narudisha tena Love Box (kitambi),” ameandika JB akiambatanisha chini picha mbili za pamoja ambazo moja inamuonyesha katika muonekano wake wa sasa akiwa na kitambi huku nyingine akiwa ni bwana mdogo mwenye mwili mwembamba.

No comments