JONAS MKUDE AJUTA KUSAINI TENA SIMBA SC... aanza kuikumbuka ofa ya Yanga

SIMBA inazidi kumfanyia unyama nahodha wake wa zamani, Jonas Mkude na taarifa kutoka kwa rafiki zake zinasema kiungo huyo anajuta kusaini klabu hiyo huku akikumbuka ofa ya Yanga.

Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo anayecheza nae Simba ni kwamba kiungo huyo hana furaha na hatua ya kuwekwa benchi.

Rafiki huyo ambaye nae anayecheza nafasi ya kiungo amesema Mkude amekasilishwa na hatua ya timu yake hususan benchi la ufundi la timu hiyo kumnyima nafasi ya kucheza hata mchezo wa kirafiki ambapo mara ya mwisho alicheza katika mchezo dhidi ya AFC Lopard akiingizwa katika kipindi cha pili.


Akiongeza alisema kwa sasa kiungo huyo ameanza kujuta kwa nini alichelewa kukubali ofa ya kujiunga Yanga ambayo ilimuwekea kiasi kikubwa cha fedha na gari lakini akabadili mawazo katika dakika za mwisho na kusaini Simba ambayo sasa inamtesa.

No comments