JOSE MARA: KINACHOIKUMBA DANSI NI UPEPO TU, UTAPITA


Bosi na mwimbaji wa Mapacha Music Band, Jose Mara amesema ugumu wa soko unaoukumba muziki wa dansi, ni upepo tu, utapita.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM wiki iliyopita, Jose Mara ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi hicho, akakiri kuanguka kwa muziki wa dansi lakini akasema hii si mara ya kwanza.

“Huu ni upepo na utapita, ipo siku wasanii wa bongo fleva nao watakuwa wanalalamika. Kuna wakati dansi ilikuwa juu lakini ikashuka kwa miaka kadhaa, baadae ikaibuka tena. Hata taarab imekuwa ikianguka na kuinuka, ni hali ya kawaida kwenye muziki,” alisema Jose Mara.

No comments