JOSE MOURINHO ASEMA LUKUKU ANAMSHANGAZA


JOSE MOURINHO amekiri kuwa anashangazwa na mshambuliaji wake mpya Romelu Lukaku.
Matarajio makubwa yamewekwa kwa nyota huyo wa Ubelgiji baada ya kufunga magoli 51 katika misimu miwili iliyopita akiwa na Everton.
Tayari Lukaku kishapachika mabao sita kwa United katika mechi sita za Premier League sambamba na bao moja la Champions League.
Lakini Mourinho, kocha wa Manchester United anasema anaduwazwa na uwezo wa mshambuliaji huyo.
"Nilikuwa nafahamu kuwa atafunga magoli mengi zaidi akiwa na United kuliko ilivyokuwa kwa Everton na West Bromwich, lakini sikutegemea kuwa angekuwa anafunga katika kila mechi," anaeleza Mourinho.No comments