JOSE MOURINHO ATAKA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WAMPE ROONEY HESHIMA YAKE LAKINI ....


Jose Mourinho amewataka mashabiki wa Manchester United wamkaribishe kwa heshima zote nahodha wao wa zamani Wayne Rooney ambaye Jumapili hii atarejea Old Trafford.
Rooney anarejea Old Trafford kuikabili Manchester United katika mchezo wa Premier League akiwa na timu yake nyingine ya zamani Everton.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rooney kurejea Old Trafford tangu alipotua Everton dirisha la kiangazi. Mchezaji huyo ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji mwenye magoli mengi kuliko yeyote yule katika historia ya Manchester United.
Jose Mourinho amewataka mashabiki wa United kuheshimu mafanikio hayo ya Wayne Rooney kabla na baada ya mchezo wao na Everton - na sio ndani ya mchezo.
Kocha huyo wa United amesema: "Nadhani atapata mapokezi yanayostahili. Idadi ya mechi alizocheza, magoli aliyofunga, mataji ni kiashiria tosha cha mchezaji muhimu katika historia ya Manchester United.

"Naamini Old Trafford itamwonyesha heshima inayostahili, natumai itakuwa ni kabla na baada ya mchezo, sio wakati mechi inaendelea".


No comments