JULIO AIONYA SIMBA SC KUHUSU KUIDHARAU YANGA KWENYE LIGI

KOCHA wa zamani wa timu ya Simba, Jamhuri Kihwelo “Julio” ameishangaa klabu hiyo kwa kujitangazia ubingwa huku wakisahau namna ambavyo Yanga walipindua msimamo wa Ligi na kutangaza ubingwa wa tatu mfululizo msimu uliopita.

Julio alisema kuwa mashabiki wa Simba wanajidanganya na matokeo ya mechi moja huku wakidhania Yanga haiku kwenye mbio za ubingwa baada ya kupata matokeo ya sare ya bao 1-1 na Lipuli.

“Huu sio msimu wa kwanza kwa Simba kuanza vizuri, lakini tatizo lao ni namna ya kumalizia Ligi na hapo ndipo Yanga wanaposhangaza, kwasababu hata mwaka jana hali ilikuwa kama hivyo,” alisema Julio.

“Simba wasijidanganye, Ligi bado mbichi na lolote linaweza kutokea. Sijui kwanini mashabiki wanasahau haraka kilichotokea msimu uliopita, hawa Yanga wanaweza kurudia walichokifanya msimu uliopita,” aliongeza.


Mashabiki wa Simba msimu uliopita waliinama vichwa chini baada ya Yanga kulifikia pengo la alama nane lililowekwa na kutangaza ubingwa katika namna ya kushangaza.

No comments