JURGEN KLOPP AMEMTETEA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemtetea mchezaji wake mpya Alex Oxlade-Chamberlain huku pia akisema klabu haipo kwenye mgogoro wowote kufuatia mwendo wao wa kusuasua tangu msimu huu uanze.

Tangu atue Liveropool msimu huu akitokea Arsenal, Oxlade-Chamberlain bado hajaonyesha ubora wake katika mechi chache alizoccheza.

Klopp amesema Ox alikuwa na wasaa mzuri mfupi na muda mfupi usio na bahati na hiyo ndiyo soka. "Hakuwa kwenye kiwango bora, lakini huo ndiyo ulimwengu wa soka. Sina mashaka naye kabisa," aliongeza kocha huyo.No comments