KAMUSOKO FITI KUIVAA MAJIMAJI

KIUNGO wa Yanga, Thabani kamusoko ameanza mazoezi na timu yake baada ya kuumia Jumapili katika mchezo wa Ligi KuuTanzania bara dhidi ya wenyeji Njombe Mji.

Kamusoko alitoka uwanjani anachechemea baada ya kuumia nyonga Jumapili na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mpya, Raphael Daud dakika ya 49 ambapo siku hiyo Yanga ilishinda bao 1-0 ugenini.

Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga, Dismas Ten, Mzimbabwe huyo alianza kufanya mazoezi na wenzake uwanja wa kiwanda cha Chai, Njombe kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Majimaji Jumamosi Songea.

Katika mazoezi hayo, mchezaji huyo wa zamani wa FC Platnums ya Zimbabwe, Mzambia Obrey Chirwa  nae amefanya mazoezi kikamilifu.

Kwa mara ya kwanza msimu huu Chirwa alitokea benchi kipindi cha pili kwenda kumpokea Donald Ngoma Jumamosi katika mchezo wa ugenini pia dhidi ya Njombe Mji, bao la Ibrahim ajib likiipa Yanga ushindi wa 1-0.


Baada ya hapo mchezaji aliyeumia Julai, mwaka huu, juzi na jana alifanya mazoezi kikamilifu kuelekea mechi na Majimaji.

No comments