KANJIBAI WA SINGELI ALILIA AMANI BONGO

MSANII anayekuja juu kwa kasi katika muziki wa singeli Bongo, Mussa Juma ‘Kanjibai’, Jumamosi hii anatarajiwa kutambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Amani’, ambayo mwenyewe anaisifu kuwa itakuwa moto wa kuoteambali.

Katika mazungumzo maalum na Saluti5, Kanjibai  amesema kuwa kibao hicho kimebeba ujumbe mzito kuhusiana na kilio cha wengi juu ya amani Bongo.

“Gumzo limekuwa kubwa hapa nchini kwa sasa kutokana na mtikisiko wa amani na umoja kwa Watanzania wengi kulalamikia matukio yanayotokea mara kwa mara yakidaiwa kufanywa na watu wasiojulikana,” amesema kanjibai.

“Hivyo nikaona iko haja ya kuandaa kazi hii ili kumuomba Mungu atujalie kurudisha hali ya utulivu miongoni mwetu kwani nafikiri hali imeanza kuwa si nzuri sana katika taifa letu kutokana na umoja kuanza kupotea,” ameongeza msanii huyo.


Kabla ya kuibuka na kibao hicho cha ‘Amani’, Kanjibai aliachia ‘Mama’ na ‘Wivu’ ambavyo vyote vilitokea kuwashika vilivyo mashabiki na wapenzi wa miondoko ya singeli Bongo.

No comments