KASI ALIYOANZA NAYO IBRAHIM AJIBU YANGA YAWASHITUA MASHABIKI WA SIMBA

MASHABIKI wa Simba wameonekana kuanza kushitushwa na kuanza kufunga kwa mshambuliaji wao wa zamani, Ibrahim Ajibu na sasa wanaonekana kukosa raha kila wanaposikia jina la mshambuliaji huyo.

Ajibu alianza kasi yake mwishoni mwa wiki iliyopita akiwapiga Njombe Mji bao 1-0 akilifunga kwa ufundi wa mpira wa adhabu ndogo.

Uchunguzi umebaini kwamba mashabiki wa Yanga kila wanampomtaja Ajibu kwa wenzao wa Simba wamekuwa wakinyamaza kimya na kukosa la kusema.

Kinachowatesa Simba ni kutokana na kugundua kwamba kasi yao ya kuwafunga Ruvu Shooting mabao 7-0 ilitokana na ukweli kuwa kikosi hicho kiliwakosa wachezaji wao muhimu na kwamba kasi yao ya kufunga ilikwama walipokutana na Azam huku Ruvu ikiwazuia Kagera ugenini walipotoka sare ya bao 1-1 baada ya wachezaji wake kurudi.

Wakati Simba wakiteswa na hilo, tayari huku nyuma Ajib ameongezewa kasi zaidi akipewa mazoezi maalum ya kuelewana na Obrey Chirwa na kwamba mambo matamu zaidi yameanza kuonyesha dalili ya kusogea.


Kasi hiyo ya Ajib inaweza sasa kuziangamiza zaidi timu pinzani kuanzia kwa Majimaji wanaokutana nao Jumamosi hii, kwenye uwanja wa Majimaji, mjini Songea na kwamba utamu wa chirwa utakuwa mwiba mkali kwa mabeki wa upinzani.

No comments