KHADIJA KOPA AACHA SIMULIZI SHOO YA ZANZIBAR STARS DDC KARIAKOO

KHADIJA Kopa ambaye ni Malkia wa mipasho anayetikisa barani Afrika, Jumanne iliyopita aliwacharusha vilivyo mashabiki wake ndani ya DDC Kariakoo pale alipopanda jukwaani na kutumbuiza kwa mbwembwe za aina yake.

Kibao "Tutabanana Hapahapa" ambacho ni kati ya kazi zilizochangia kumweka juu zaidi, ndicho ambacho alianza nacho kutumbuiza siku hiyo na kuwavuta katikati ya ukumbi mashabiki wengi waliokuwa wametulia vitini mwao.

“Nawapenda sana mashabiki wangu, naipenda pia Zanzibar Stars kwasababu ni miongoni mwa bendi nilizozitumikia na kunipa heshima kubwa hapa nchini,” amesema Kopa akiongea na ripota wetu baada ya kushuka jukwaani.


Zanzibar Stars inayokusanya mastaa wengi wa mipasho na ambayo kwa sasa iko chini ya mkurugenzi Juma Mbizo, inatumbuiza ndani ya ukumbi huo wa DDC Kariakoo kila wiki, katika siku za Jumanne.

No comments